array(0) { } Radio Maisha | Raila agiza kusitishwa kwa shuguli ya uchimbaji mchanga Likoni

Raila agiza kusitishwa kwa shuguli ya uchimbaji mchanga Likoni

Raila agiza kusitishwa kwa shuguli ya uchimbaji mchanga Likoni

Mjumbe Maalum wa masuala ya muundo msingi Afrika Raila Odinga ameagiza kusitishwa mara moja kwa shughuli ya uchimbaji mchanga katika Bandari ya Mombasa ambayo imekuwa ikiendelezwa na Mamlaka ya Bandari hiyo ili kuwapa wapiga-mbizi muda mwafaka wa kutekeleza oparesheni ya kuiopoa mili ya watu watatu waliozama katika Kivuko cha Likoni.

Akizungumza muda mfupi uliopita baada ya kukutana na familia ya Mariam Kigenda aliyezama akiwa na mwanawe Amanda, , Raila ameeleza kusikitishwa na jinsi ambavyo uchimbaji huo umekuwa ukiathiri oparesheni hiyo.

Kulingana na Raila wakati huu sio mwafaka wa kulimbiziana lawama kufuatia mkasa huo akisema la msingi ni kuhakikisha mili ya waliozama inapatikana na kutolewa mara moja.

Raila ametuma risala za rambirambi kwa familia iliyopioteza wapendwa wao kufuatia mkasa huo.
Ameeleza kuridhishwa kwake na juhudi ambazo zimekuwa zikiendelezwa na vitengo mbalimbali vya wapiga-mbizi ili kuhakikisha mili ya waliozama inaopolewa.

Hayo yanajiri huku oparesheni hiyo ikiwa imetatizwa na mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha kwenye Kaunti ya Mombasa tangu asubuhi.