array(0) { } Radio Maisha | Serikali kuimarisha muundo msingi na shughuli katika bandari ya mombasa

Serikali kuimarisha muundo msingi na shughuli katika bandari ya mombasa

Serikali kuimarisha muundo msingi na shughuli katika bandari ya mombasa

Serikali imesema kwamba imeweka mikakati kuimarisha muundo msingi na shughuli katika bandari ya mombasa. Akiwahutubia wanahabari muda mfupi uliopita Waziri wa Uchukuzi James Macharia amesema tayari serikali imeagiza meli nyingine ambayo itawasili nchini Januari mwaka ujao. Aidha amesema meli nyingine tatu zitanunuliwa kati ya kipindi cha miaka minne na mitano.

Wakati uo huo, amesema wamezidisha juhudi za kuitafuta mili ya watu watatu waliozama katika kivuko hicho cha Likoni Jumapili iliyopita.

Macharia amesema wanaendelea kuvihusisha vitengo mbalimbali akisema wataalam wengine wawili wanatarajiwa kuwasili nchini kutoka Afrika Kusini ili kusaidia katika shughuli za uopoaji.

Aidha Waziri huyo amesema Idara ya Hali ya Anga imewahakikishia kuwa hali itakuwa nzuri siku tatu zijazo akisema wanalenga kutumia muda huo kuhakikisha mili hiyo inapatikana.