array(0) { } Radio Maisha | Ajali za barabarani zimepungua pakubwa - NTSA yasema

Ajali za barabarani zimepungua pakubwa - NTSA yasema

Ajali za barabarani zimepungua pakubwa - NTSA yasema

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Visa vya ajali miongoni mwa magari ya uchukuzi wa umma vimepungua mwaka huu ikilinganishwa na miaka mitatu iliyopita, huku ajali za magari ya binafsi zikiongezeka.

Ndiyo kauli ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uchukuzi na Usalama Barabarabi NTSA, Francis Meja ambaye amewalaumu madereva wa magari ya binafsi kwa kupuuza sheria za trafiki.

Akizungumza wakati wa kutoa ripoti kufuatia ajali ya eneo la Awasi, Kaunti ya Kisumu ambapo watu kumi na watatu wamefariki dunia, Meja amesema NTSA imeweka mikakati ya kuwakabili wakiukaji wa sheia za barabarani.

Meja amesema oparesheni ya kuwapokonya leseni madera wanaokiuka sheria za barabarani inaendelea kufuatia agizo la Waziri wa Uaslama Dkt. Fred Matiang'i juma lililopita alipokutana na makamanda wa maeneo mbalimbali.

Wakati huo huo kuhusu ajali ya Awasi,  Msemaji wa Polisi Charles Owino amesema kwa mujibu wa walioshuhudia, dereva wa basi alipoteza mwelekeo baada ya kukanganywa na mwangaza mkali wa taa za trela lililokuwa likiendeshwa kwa kasi.

Owino amesema abiria hamsini na mmoja walikuwa wameabiri basi hilo ili kusafiri kuja Nairobi ambapo manusura wanatibiwa katika hospitali za Ahero, ile ya Rufaa ya Jaramogi na Muhoroni.

Hata hivyo, amewasishi madereva, abiria na wapitanjia kuwa makini wanaposafiri barabarani.