array(0) { } Radio Maisha | Mahakama kuamua iwapo Sarah Cohen atawachiliwa kwa dhamana

Mahakama kuamua iwapo Sarah Cohen atawachiliwa kwa dhamana

Mahakama kuamua iwapo Sarah Cohen atawachiliwa kwa dhamana

Na Esther Kirong'

NAIROBI, KENYA, Mahakama Kuu Ijumaa inatarajiwa kuamua iwapo itamwachilia kwa dhamana au la Sarah Wairimu, mshukiwa mkuu wa mauaji ya mfanyabiashara Tob Cohen. Wairimu alifikishwa mahakamani Alhamisi ambapo alikana mashtaka ya mauaji yanayomkabili.

Hakimu Stella Mutuku anayeisikiliza kesi hiyo aidha alikataa ombi na upande wa mashtaka ukiongozwa na Cathrine Mwaniki kutaka kupewa muda zaidi ili kuwasiliana na Idara ya kuwalinda mashahidi kabla ya uamuzi wa leo kutolewa. Alisema muda ambao umekuwa ukitolewa tangu kesi hiyo kuanza ni wa kutosha kwa pande zote kujitayarisha.

Mshukiwa ataendelea kuwaklishwa na wakili wake Philip Murgor baada ya mahakama kutupilia mbali ombi lililowasilishw ana Wakili wa familia Cliff Ombeta na kuungwa mkono na upande wa mashtaka wakitaka wakili huo kujiondoa wakidai majukumu yanaingiliana kwani alikuwa akifanya kazi katika Ofisi ya Mkuu wa Mashtaka ya Umma.

Hata hivyo, mahakama ilibaini kwamba Murgor alijiuzulu mapema mwaka huu kwa kumwandikia DPP na kwamba hakuna mwingilaino wa majukumu.

Hayo yanajiri huku mshukiwa mwingine Petre Karanja akiendelea kuzuiliwa katika gereza na Industrial Area hadi tarehe kumi na moja mwezi huu atakaposomewa mashtaka.