array(0) { } Radio Maisha | Madereva wa malori kuendelea kuandamana kila Jumatatu
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Madereva wa malori kuendelea kuandamana kila Jumatatu

Madereva wa malori kuendelea kuandamana kila Jumatatu

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Madereva wa malori wameapa kuendelea na maandamano yao ya kila Jumatatu wakipinga shughuli za usafirishaji wa mizigo kupitia reli ya kisasa SGR licha ya serikali kutangaza kwamba imesitisha kwa muda usafirishaji wa lazima wa mizigo kutoka Mombasa kupitia SGR hadi hapa jijini Niarobi.

Madereva hao wanadai kwamba mazungumzo yaliyofanyika Alhamisi na Waziri wa Uchukuzi James Macharia, Waziri Fred Matiang'i na viongozi wa eneo la Pwani wakiongozwa na Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho yalikuwa kinyume na sheria ikizingatiwa agizo hilo lilitolewa bila wao kuhusishwa.

Wamesema linastahili kufutiliwa mbali kabisa kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa eneo la Mombasa. 

Alhamisi, serikali ilisema imeafikiana na viongozi hao wa eneo la Pwani kuhusu mvutano huo ikisema itaendelea na mazungumzo kutafuta mwafaka huku ikisitisha kwa muda  usafirishaji huo wa lazima wa mizigo kutoka Mombasa kupitia reli ya Kisasa, SGR ikisema agizo la Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi KRA na Mamlaka ya Bandari KPA lilitolewa bila majadiliano.

Waziri wa Uchukuzi, James Macharia aliwahakikishia viongozi hao kwamba kuwa agizo la kusitisha usafirishaji huo lilitolewa awali na litasalia, akisisitiza serikali itazidi kuimarisha Bandari ya Mombasa.

Gavana wa Mombasa, Ali Hassan Joho kwa upande wake alisemaSGR ni mradi ambao utakuwa wa manufaa sio tu kwa wakazi wa Mombasa bali wa taifa zima iwapo itaendeshwa vyema.