array(0) { } Radio Maisha | Abiria 14 wafariki dunia katika ajali eneo la Awasi

Abiria 14 wafariki dunia katika ajali eneo la Awasi

Abiria 14 wafariki dunia katika ajali eneo la Awasi

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Watu kumi na wanne wamefariki dunia usiku wa kuamkia Ijumaa baada ya basi lililokuwa likitoka Kisumu kuja hapa Nairobi kugongana ana kwa ana na trela kwenye eneo la Awasi, Kaunti ya Kisumu.

Aidha ,watu wengine thelathini na wanane wamejeruhiwa vibaya katika ajali hiyo ya saa saba usiku.

Kamanda wa Trafiki Gladys Ogonda, amesema watu kumi na watatu walifariki papo hapo huku mmoja akifariki akipelekwa hospitalini.

Ogonda amewashauri madereva kuwa waangalifu hasa usiku ili kuepuka ajali. Kamanda wa Polisi wa Kisumu, Benson Maweu amesema mili ya kumi na wanne hao imelazwa katika hospitali za Ahero, Jaramogi na Muhoroni huku waliojeruhiwa wakiendelea kutibiwa katika hospitali zizo hizo.

Inaarifiwa kufikia saa tisa leo alfajiri, dereva wa basi hilo alikuwa angali ndani ya gari hilo. Polisi bado hawajathibitisha idadi ya abiria waliokuwa wakisafiri kutumia basi hilo la Kampuni ya Eldoret Express.

Aidha kwa mujibu wa manusura ambao wanaendelea kutibiwa, dereva wa gari hilo alikuwa akiendesha kwa kasi mno.