array(0) { } Radio Maisha | Sarakasi za Kiambu zachacha huku Naibu Gavana akitaka Mahakama kumuruhusu kulifanyia marekebisho baraza la mawaziri

Sarakasi za Kiambu zachacha huku Naibu Gavana akitaka Mahakama kumuruhusu kulifanyia marekebisho baraza la mawaziri

Sarakasi za Kiambu zachacha huku Naibu Gavana akitaka Mahakama kumuruhusu kulifanyia marekebisho baraza la mawaziri

Naibu Gavana wa Kiambu James Nyoro sasa anaitaka Mahakama ya Uajiri na Leba kuondoa agizo linalomzuia kulifanyia marekebisho Baraza la Mawaziri katika serikali ya Kaunti hiyo akisema kwamba agizo hilo linazuia kutolewa kwa huduma kwa wakazi wa eneo hilo.

Kupitia wakili Kibe Mungai, Nyoro amesema kwamba hakuna sababu kuu iliyotolewa na mahakama hiyo ya kumzuia kutekeleza mabadiliko hayo.

Ikumbukwe kuwa Jaji Onesmus Makau alimzuia Nyoro kutekeleza mabadiliko yoyote kwenye uongozi wa Kaunti ya Kiambu miezi miwili baada ya Gavana wa Kiambu Ferdinard Waititu kuzuiwa na Mahakama Kuu kuripoti ofisini mwake kwa kuhusishwa na ufisadi.