array(0) { } Radio Maisha | Wapiga-mbizi waendelea na shughuli ya kuitafuta mili Bahari Hindi

Wapiga-mbizi waendelea na shughuli ya kuitafuta mili Bahari Hindi

Wapiga-mbizi waendelea na shughuli ya kuitafuta mili Bahari Hindi

Kufikia sasa, jumla ya maeneo sita yaliyokuwa miongoni mwa maeneo yanayokisiwa huenda gari iliyozama ikiwa na watu watatu katika Kivuko cha Likoni ilikwama yamefanyiwa ukaguzi na Wapiga-Mbizi wanaoongoza na Jeshi la Wanamaji.

Msemaji wa Serikali Kanali Mstaafu Cyrus Oguna amesema kwamba leo wapiga mbizi wataendelea kuyakagua maeneo mengine manane ambayo yamesalia.

Ameeleza matumaini ya eneo ambalo gari hiyo imekwama kupatikana huku akisema endapo ukaguzi katika maeneo hayo utakamilika bila gari hiyo kupatikana basi mikakati zaidi itawekwa kuendelea kuitafuta ilipo.

Amesema kwamba Serikali inaendelea kuwajibika kuhakikisha miili ya watu watatu waliozama akiwamo Mariam Kigenda na mwanamwe Amanda Mutheu inaopolewa.

Shughuli za Uchukuzi katika Kivuko hicho inatarajiwa kusitishwa kwa takriban masaa mawili muda wowote kuanzia sasa ili kuwapa fursa wapiga mbizi wanaoongozwa na Mkuu wa Jeshi la Wanamaji Lawrence Gituma kuendelea kuitafuta gari hiyo.

Maeneo hayo kumi na manne ni ambayo yalinakiliwa na mitambo ya angani kupitia ndege maalum iliyokagua Kivuko hicho.