array(0) { } Radio Maisha | Wabunge na maseneta wawalaumu wasimamizi wa feri kufuatia utepetevu
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Wabunge na maseneta wawalaumu wasimamizi wa feri kufuatia utepetevu

Wabunge na maseneta wawalaumu wasimamizi wa feri kufuatia utepetevu

Kuendelea kuwepo ofisini kwa wakuu wa Shirika la Feri Nchini pamoja na Waziri wa Uchukuzi James Macharia ni kejeli kwa familia za watu watatu waliozama katika Kivuko cha Likoni siku nne zilizopita huku wahusika wakionekana kutotikisika kivyovyote na tukio hilo.

Ilivyo ada humu nchini, viongozi hao wataendelea kuitisha vikao na wanahabari kutoa taarifa za kuzifariji familia za waathiriwa na baadae kisa hicho kusahaulika huku kufikia sasa ikiwa haijulikani iwapo serikali yetu tukufu itafanikiwa kuiopoa miili ya waliozama baharani humo Jumapili jioni.

Ni wakati wahusika waajibishwe na hatua za dharura kuchukuliwa ili kuepuka visa sawa na hivyo katika siku za usoni ikizingatiwa shughuli chungu nzima ambazo hushuhudiwa kwenye kivuko hicho usiku na mchana.

Jana, Maspika wa Mabunge ya Kitaifa na Seneti Justin Muturi na Ken Lusaka, walisitisha shughuli za kawaida za bunge na kuwaruhusu Wabunge na Maseneta kujadili usalama wa safari za baharini. Ni mjadala ambao uliibua hisia kinzani huku wabunge na masenetea hususan wa eneo la Pwani wakielezea kukerwa kwao na tukio hilo.Mishi Mboko ni Mbunge wa Likoni.

Aidha, suala la kukithiri kwa ufisadi kumetajiwa kuchangia katika ukosefu wa kufanikiwa kuiopoa mili ya watu watatu waliozama, pamoja na kwamba watu wanaoajiriwa katika kitengo cha jeshi la wanamaji na walinzi wa Baharini Kenya Coast Guard na vingine hawana ujuzi wowote wa kupiga mbizi.

Suala lilo hilo lilijadiliwa kwa kina kwenye Bunge la Seneti huku suala la ukosefu wa maafisa wa kukabili majanga ya dharura kwenye feri likionekana kuwakera maseneta.