array(0) { } Radio Maisha | Sportpesa yasitisha shughuli zake nchini

Sportpesa yasitisha shughuli zake nchini

Sportpesa yasitisha shughuli zake nchini

Huenda klabu za humu nchini zilizokuwa zikifadhiliwa na kampuni za michezo ya bahati nasibu, SportPesa na Betin Kenya zikaathirika hata zaidi baada ya kampuni hizo kusitisha shughuli zake nchini huku wamiliki wakiilaumu serikali kufuatia mazingira duni ya kufanyia kazi.

Tangazo hilo linajiri baada ya uamuzi wa serikali kuwatoza asilimia ishirini ya mapato yake kuwa kodi, hatua ambayo kampuni hiyo imesema kuwa inalenga kuzikandamiza shughuli zake vilevile kwa wateja wake.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Sportpesa imeeleza kusikitishwa na hatua ya bunge kupitisha sheria hiyo ikisema kuwa ilichochewa na Wizara ya Fedha kukosa kuelewa jinsi kampuni hizo zinavyopata mapato yake.

Aidha imesema kuwa haitarejelea shughuli zake hadi pale sheria ya kodi ya asilimia ishirini itakapoangaziwa upya vilevile kuwekwa kwa sheria zitakazoboresha biashara ya mchezo huo.

Ikumbukwe jana Kampuni ya Betin iliwaambia wafanyakazi wake kwamba kufuatia mazingira magumu ya kuendesha biashara yao haina budi ila kusitisha shughuli zake nchini hivyo kuwaachisha kazi.

Usimamizi wa Betin umekuwa ukishiriki mikutano mara kwa mara na serikali kuhusu kuidhinishwa upya kwa leseni ya kuhudumu kabla ya uamuzi wa jana.