array(0) { } Radio Maisha | Kuria amtaka Murkomen kujiuzulu wadhfa wa kiongozi wa wengi katika seneti

Kuria amtaka Murkomen kujiuzulu wadhfa wa kiongozi wa wengi katika seneti

Kuria amtaka Murkomen kujiuzulu wadhfa wa kiongozi wa wengi katika seneti

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria, amemtaka Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen kujiuzu wadhifa wa Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Seneti. Kuria amemshauri Murkomen kuondoka katika nafasi hiyo kutokana na kauli yake ya kupinga kusitishwa kwa mradi wa ujenzi wa Bwawa la Kimwarer.

Mbunge huyo anataka uongozi wa Chama cha Jubilee kumwadhibu Seneta Murkomen ambaye amepinga hatua ya Rais Kenyatta kuusitisha mradi huo akisema kwamba umeshinikizwa na jamii fulani.

Kuria ametaja matamshi ya Murkomen kuwa ya ukabila, akisema ipo miradi mingi hata kwenye eneo la kati ambayo imesitishwa.

Jana, Rais Kenyatta aliagiza kusitishwa kwa mradi huo baada ya kupokea ripoti ya kamati maalum iliyobuniwa kutathmini miradi wenyewe, baada ya kuibuliwa kwa madai ya ufisadi.

Kufuatia agizo hilo la rRais katika taarifa kwenye mtandao wa twitter, Murkomen alimkosoa Rais akidai ni kwamba ni njama ya kusambaratisha miradi ya maendeleo kwenye eneo la Elgeyo Marakwet.