array(0) { } Radio Maisha | Washukiwa watatu ambao wamepatikana leo hii wakipakia mchele ambao muda wa kutumika umekamilika

Washukiwa watatu ambao wamepatikana leo hii wakipakia mchele ambao muda wa kutumika umekamilika

Washukiwa watatu ambao wamepatikana leo hii wakipakia mchele ambao muda wa kutumika umekamilika

Kikosi cha Pamoja cha kukabili ufisadi katika eneo la Kamukunji Jijini Narobi, kimewanasa washukiwa watatu ambao wamepatikana leo hii wakipakia mchele ambao muda wa kututumika umekamilika.

Washukiwa Abdikafi Ahmed, Abdirizack Ahmed na Liban Ahmed Abdille wametiwa nguvuni wakiwa na mchele huo magunia elfu moja na mia tano ya kilo tisini.

Afisi ya Idara ya Upelelezi DCI, imesema mchele huo umenaswa pamoja na lori na bidhaa nyingine.


Washukiwa watafikishwa mahakamani punde uchunguzi dhidi yao utakapokamilika.