array(0) { } Radio Maisha | Rais Kenyatta atangaza kumuunga Mariga

Rais Kenyatta atangaza kumuunga Mariga

Rais Kenyatta atangaza kumuunga Mariga

Rais Uhuru Kenyatta amemhakikishia Macdonald Mariga kuwa atamuunga mkono katika kampeni zake za kuwania ubunge wa Kibra kwenye uchaguzi mdogo wa tarehe 7/11/2011

Kenyatta ambaye ni Kinara wa Jubilee, ametoa hakikisho hilo baada ya kufanya kikao na Naibu wa Rais Dkt. William Ruto katika ikulu,  ajenda kuu ikiwa jinsi ya kuhakikisha Mariga mwenye tiketi ya Jubilee ataibuka mshindi kwenye uchaguzi huo.

Ikiwa njia mojawapo ya kudhihirisha umoja uliopo miongoni mwa vigogo wa Jubilee licha ya madai ya migawanyiko kuibuka awali, Katibu Mkuu wa chama hicho Raphael Tuju, Kiongozi wa Wengi katika bunge la Kitaifa Aden Duale na Kiranja wa Bunge Benjamin Washiali waliandamana na Mariga wakati wa kikao hicho.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha ODM Edwin Sifuna kuwaongoza wanachama wa ODM kumpigia debe mwaniaji wake wa kiti cha Kibra, Imran Okoth katika maeneo mbalimbali ya Kibra.

Aidha Eliud Owalo wa ANC alizuru maeneo mbalimbali na hata kumsadia ajuza mmoja kujenga nyumba wakati wa kampeni yake.

Kinyang'anyiro hicho kinatarajiwa kutawaliwa na kampeni kali ambapoMariga wa Jubilee atamenyana na Imran wa ODM, Eliud Owalo wa ANC, Khamisi Butichi wa Ford Kenya miongoni mwa wengine.