array(0) { } Radio Maisha | Spika Oloo wa Kisumu afurushwa

Spika Oloo wa Kisumu afurushwa

Spika Oloo wa Kisumu afurushwa

Bunge la Kaunti ya Kisumu limepitisha hoja ya kumng'oa mamlakani Spika Onyango Oloo.

Wawakilishi wadi 42 wameunga mkono hoja iliyowasilishwa na Mwakilishi Wadi ya Kondele, Joachim Oketch

Haya yalijiri saa chache tu baada ya Spika huyo kuzuiliwa kuingia katika ofisi za bunge hilo.

Spika huyo amefurushwa Kwa madai ya Ufisadi na upendeleo katika kazi yake.

Wiki iliyopita Onyango Oloo alifikishwa mahakamani kwa mashtaka ya ufisadi ambapo aliyakana.

Onyango Oloo aliachiliwa kwa dhamana ya milioni 10