array(0) { } Radio Maisha | Rais asitisha ujenzi wa mabwawa ya Kimwarer na Arror

Rais asitisha ujenzi wa mabwawa ya Kimwarer na Arror

Rais asitisha ujenzi wa mabwawa ya Kimwarer na Arror

Rais Uhuru Kenyatta ameagiza kusitishwa mara moja kwa miradi ya ujenzi wa Mabwawa ya Arror na Kimwarer.

Agizo hilo limejiri baada ya Rais kupokea ripoti ya kamati maalumu iliyobuniwa kutathimini miradi hiyo baada ya kuibuliwa kwa madai ya ufisadi ambapo imependekeza miradi hiyo kusitishwa.

Kamati hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Katibu wa Wizara ya Muundo Msingi Paul Maringa ilijukumiwa kuchunguza kiwango cha fedha kilichotolewa kuitekeleza miradi hiyo kisha kutakiwa kuwasilisha Ripoti katika kipindi cha siku thelathini.

Aidha uchunguzi wa kamati hiyo ulibaini kuwa eneo ambapo bwawa hilo lilitarajiwa kujengwa halikuwa limefanyiwa tathmini yoyote. Tathmini ya mwisho ilifanyika miaka ishirini na minane iliyopita.

Aidha ilibainika kwamba eneo hilo ni sehemu ya makazi ya watu ambapo wenyeji wangehitajika kufidiwa kabla ya mradai huo kutekelezwa.

Kuhusu mradi wa ujenzi wa bwawa la Arror; japo ilibainika kuwa mradi huo ulifaa, gharama yake vile vile iliongezwa kuliko inavyostahili.

Hata hivyo kamati hiyo imesema itakuwa rahisi kuutekeleza mradi huo kwani utahitaji tu ekari mia mbili hamsini za ardhi na gharama ya shilingi bilioni 15.4 kinyume na shilingi bilioni 28.2 ilivyodaiwa awali.