array(0) { } Radio Maisha | Mwanamuziki Akothee azua sarakasi na minisketi bungeni

Mwanamuziki Akothee azua sarakasi na minisketi bungeni

Mwanamuziki Akothee azua sarakasi na minisketi bungeni

Mwanamuziki Esther Akoth maarufu Akothee aliibua sarakasi katika jengo la Bunge la Kitaifa baada ya maafisa wa usalama kumzuia kuingia ndani ya bunge hilo, kwa misingi ya kutovalia nadhifu inavyopaswa kisheria.

Akothee ambaye alikuwa ameenda kupatana na mbunge maalumu David Sankok, aliruhusiwa kuingia katika mkahawa wa bunge hilo pekee kinyume na matarajio yake .

Baada ya kujibizana vikali kwa muda wa dakika tano akisukumana na walinzi wa bunge langoni, Akothee aliyekuwa amevalia minisketi iliyodaiwa kutosetiri mwili wake, alifurushwa na maafisa hao kupitia lango la nyuma ya bunge.

Akothee aliwakashifu walinzi hao akisema kwa mujibu wake nguo alizovalia zilikuwa rasmi.