array(0) { } Radio Maisha | Afisa wa Upelelezi wa binafsi, Jane Mugo anayedaiwa kutekeleza uhalifu aachiliwa uhuru

Afisa wa Upelelezi wa binafsi, Jane Mugo anayedaiwa kutekeleza uhalifu aachiliwa uhuru

Afisa wa Upelelezi wa binafsi, Jane Mugo anayedaiwa kutekeleza uhalifu aachiliwa uhuru

Afisa wa Upelelezi wa binafsi, Jane Mugo ambaye anadaiwa kutekeleza visa vya uhalifu kwa kujidai kuwa afisa wa ujasusi, ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu mia tatu au shilingi elfu mia tano pesa taslimu.

Mugo ambaye amefikishwa mbele ya Hakimu Mkuu Francis Andayi anashukiwa kuwatishia maisha Patrick Mugusia Kefa na Deepa Shah.

Siku iliyotangulia Jane alisema maisha yake yamo hatarini huku Kiongozi wa Idara ya Uchunguzi katika KNHCR, Kamanda Mucheke akiwashauri maafisa wa Idara ya Upelelezi, DCI kufuata sheria wakati wa kumkamata Mugo.

Mugo ambaye alikuwa mafichoni hata hivyo anasisitiza kwamba polisi wanamhangaisha baada ya kubaini uchunguzi wake unalenga kufichua visa vya ufisadi miongoni mwa maafisa wakuu wa Idara ya Polisi.