array(0) { } Radio Maisha | Rais Kenyatta awasihi viongozi wa Afrika kubuni nafasi za ajira

Rais Kenyatta awasihi viongozi wa Afrika kubuni nafasi za ajira

Rais Kenyatta awasihi viongozi wa Afrika kubuni nafasi za ajira

Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza haja ya viongozi wa Bara la Afrika kushirikiana katika kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kufanikisha ujenzi wa viwanda vya kutoa ajira kwa vijana.

Akihutubu wakati wa Kongamano la Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi Barani Afrika Jijini Nairobi, Kenyatta amesikitia hali ambapo Waafrika wengi wanatesekea ughaibuni wakitafuta riziki kufuatia uhaba wa nafasi za ajira.

Kuhusu mfumo wa teknolojia ambao waajiri wengi wameukumbatia ili kuboresha uzalishaji viwandani, Kenyatta amesema waajiri wanafaa kuhakikisha teknolojia haupunguzi nafasi za ajira kwani asilimia kubwa ya watu wanahitaji ajira.

Wakati uo huo Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi COTU Francis Atwoli amempongeza Rais Kenyatta kwa kuangazia maslahi ya wafanyakazi kupitia ajenda zake kuu nne.