array(0) { } Radio Maisha | Sonko awaachisha kazi wahudumu 2 wa afya

Sonko awaachisha kazi wahudumu 2 wa afya

Sonko awaachisha kazi wahudumu 2 wa afya

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amewaachisha kazi kwa muda wauguzi 2 wanaohudumu katika Kituo cha Afya cha Dandora Health Centre kufuatia ripoti kwamba mwanamke mmoja alijifungua mwanawe nje ya hospitali hiyo kwa kukosa shilingi ishirini pekee za kujisajili.

Aidha, Sonko ameagiza uchunguzi wa kina kufanyika kuhusu suala hilo huku akitaka kupewa majibu kabla ya kufikia leo jioni.

Wakati uo huo, Waziri wa Afya kwenye Kaunti ya Nairobi Mohammed Dagane amesema wauguzi hao watachukuliwa hatua za kisheria iwapo watapatikana na hatia.