array(0) { } Radio Maisha | Ruto amlaumu Raila kwa masaibu ya Jubilee

Ruto amlaumu Raila kwa masaibu ya Jubilee

Ruto amlaumu Raila kwa masaibu ya Jubilee

Naibu wa Rais Dkt. William Ruto ameendelea kumlaumu Kiongozi wa ODM, Raila Odinga kwa masaibu yanayokikumba Chama cha Jubilee.

Akizungumza wakati wa misa ya mazishi ya babaye Seneta wa Meru, Mithika Linturi, kwenye Kaunti ya Meru, Ruto amesema masaibu ya Chama cha Jubilee yalianza punde tu Rais Kenyatta alipopatana na Raila wakati wa 'handshake'

Ruto amemlaumu Raila kwa kutumia mijadala ya kuifanyia katiba marekebisho hali ambayo imesambaratisha shughuli za Jubilee.

Ikumbukwe kabla ya handshake, Rais alikuwa ameitisha mkutano wa wabunge wa Jubilee mwaka 2017 ambapo aliwaonya dhidi ya kufanya siasa hadi mwaka 2021. Badala yake Kenyatta aliwataka kuangazia ajenda yake ya maendeleo.