array(0) { } Radio Maisha | Washukiwa wizi wa shilingi milioni 42 za Benki ya Equity wataendelea kuzuiliwa kwa siku kumi

Washukiwa wizi wa shilingi milioni 42 za Benki ya Equity wataendelea kuzuiliwa kwa siku kumi

Washukiwa wizi wa shilingi milioni 42 za Benki ya Equity wataendelea kuzuiliwa kwa siku kumi

Washukiwa wawili wa wizi wa shilingi milioni 42 za Benki ya Equity wataendelea kuzuiliwa kwa kipindi cha siku kumi ili polisi kukamilisha uchunguzi wao.

Wawili hao; Roba Diba Boru, ambaye ni Meneja wa Shughuli za Benki hiyo tawi la Moyale na Lang'at Kipng'etich Nelson ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Ulinzi ya Wells Fargo wamefikishwa mahakamani ambako walikana mashtaka dhidi yao.

Ikumbukwe kuwa Diba na Lang'at walikamatwa na maafisa wa Idara ya Upelelezi, DCI mjini Moyale na kuachiliwa kabla ya kukamatwa tena na kusafirishwa hadi jijini nairobi walikofunguliwa mashtaka.

Taarifa hii inajiri siku moja tu baada ya polisi kumkamata mshukiwa mwingine anayehusishwa na wizi wa milioni 72 za benki ya Standard Chartered tawi la Nairobi West. Bernard Sewanga, mfanyakazi wa kampuni ya G4S kwenye nyumba mpya aliyokodisha kwenye maeneo ya Ruiru anakodaiwa kuwa mafichoni baada ya wizi huo baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi.