array(0) { } Radio Maisha | Rais Uhuru Kenyatta amesafiri Singapore kwa ziara rasmi.

Rais Uhuru Kenyatta amesafiri Singapore kwa ziara rasmi.

Rais Uhuru Kenyatta amesafiri Singapore kwa ziara rasmi.

Rais Uhuru Kenyatta amesafiri kuelekea taifa la Singapore ambako ameratibiwa kuhutubu katika kongmanao la Sigapore Summit Ijumaa na Jumamosi wiki hii katika Hoteli ya Shangri-La.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Msemaji wa Ikulu Kanze Dena amesema kwamba Uhuru amesafiri kufuatia mwaliko wa Waziri Mkuu wa Singapore Le Hsein Loong.

Katika hotuba yake, Uhuru anatarajiwa kuzungumzia hatua Kenya imepiga kiuchumi pamoja miradi ya maendeleo katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Ikumbukwe kuwa kongamano hilo linawaleta pamoja marais, viongozi wa sekta za binafsi na waekezaji kutoka mataifa mbalimbali duniani lengo kuu likiwa kujadili masuala ya biashara, fedha na miradi ya maendeleo.

Baadaye, Uhuru anatarajiwa kusafiri hadi Marekani ambako ataungana na marais wengine kuhudhuria Kongamano la 74 la Umoja wa mataifa, UNGA, jijini New York tarehe 24 mwezi huu.