array(0) { } Radio Maisha | Gavana Alfred Mutua atajwa wa kwanza katika utendakazi huku Waititu akiorodeshwa wa mwisho

Gavana Alfred Mutua atajwa wa kwanza katika utendakazi huku Waititu akiorodeshwa wa mwisho

Gavana Alfred Mutua atajwa wa kwanza katika utendakazi huku Waititu akiorodeshwa wa mwisho

Gavana wa Machakos Dakta Afred Mutua ametajwa kuwa gavana mchapakazi kote nchini huku Gavana wa Kiambu Ferdinard Waititu akiorodheshwa kuwa mwisho miongoni mwa Magavana.

Shirika moja la Uingereza  All Africa Advisors limetaja Gavana mutua kuwa bora katika utendakazi, akifuatwa na mwenzake wa Kakamega Wycliffe Oparanya na kisha Gavana wa Nairobi Mike Sonko akitwaa nafasi ya tatu.

Katika utafiti wake wa hivi punde uliofanywa kati ya Juni na Agosti, shirika hilo, limemtaja Gavana wa Makueni Profesa Kivutha Kibwana kuwa katika nafasi ya nne katika utendakazi huku Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho akishikilia nafasi ya tano.

Shirika  la All Africa Advisors ambalo linashughulikia masuala ya uchumi na miradi ya maendeleo Afrika, limemorodhesha Gavana wa Kiambu Ferdinand Waitutu kuwa gavana mwenye utendakazi mbaya kote nchini.

Shirika hilo aidha limetaja kuboreshwa kwa miundo- msingi kuwa ajenda kuu ya maendeleo katika maeneo bunge mengi nchini ikiwa njia moja wapo ya kuboresha maendeleo mashinani.