array(0) { } Radio Maisha | Washukiwa watatu wa wizi wa magari wanazuiliwa Eldoret

Washukiwa watatu wa wizi wa magari wanazuiliwa Eldoret

Washukiwa watatu wa wizi wa magari wanazuiliwa Eldoret

Washukiwa watatu wanazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Central Mjini Eldoret kwa madai ya kuhusika na wizi wa magari.


Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi katika Kaunti ya Uasin Gishu Johnston Ipara washukiwa zaidi ambao wanadaiwa kujihusisha na wizi wa magari katika mji wa Eldoret wanasakwa waliokamatwa wakitarajiwa kufikishwa mahakamani.


Aidha Ipara amewataka wale ambao wana habari zozote kuhusiana na visa hivyo kuripoti kwa Kituo cha Polisi ili kuhakikisha kuwa wahusika wanakamatwa.


Kwa zaidi ya mwaka mmoja wenyeji wa Mji wa Eldoret wamekuwa wakilalamikia visa vya magurudumu na magari yao kuibiwa na kundi lisilojulikana.