array(0) { } Radio Maisha | Baraza la Wazee Kirinyaga limeshutumu vikali kuzomewa kwa Gavana wa eneo hilo Anne Waiganjo katika mji wa Kagumo

Baraza la Wazee Kirinyaga limeshutumu vikali kuzomewa kwa Gavana wa eneo hilo Anne Waiganjo katika mji wa Kagumo

Mwenyekiti wa Baraza hilo Cyrus Githaka ametishia kuwalaani vijana waliomzomea gavana huyo iwapo hawataomba msamaha hadharani kwa kukosa kumheshimu kiongozi wao.

Akiwahutubia wanahabari kwenye eneo la Riagitugu wakati wa hafla ya kuidhinishwa kwa aliyekuwa Mbunge wa Mwea Peter Gitau kuwa mwanachama wa baraza hilo, Githaka amesema kwamba tayari wamebaini kuwa wafuasi wa Mwakilishi Wadi ya Mutira, Kinyua Wangui ndio waliohusika wakati wa mkutano huo.

Ikumbukwe kuwa vijana waliokuwa wakihudhuria mkutano huo walimzumea gavana Waiganjo wakitaka Mwakilishi Wadi huyo kupewa fursa ya kuwahutubia wakati wa ufunguzi wa soko la kisasa la Kagumo.