array(0) { } Radio Maisha | Bima ya Shilingi bilioni 1.7ya Kaunti ya Nairobi imeangaziwa katika ripoti ya uhasibu

Bima ya Shilingi bilioni 1.7ya Kaunti ya Nairobi imeangaziwa katika ripoti ya uhasibu

Bima ya Shilingi bilioni 1.7ya Kaunti ya Nairobi imeangaziwa katika ripoti ya uhasibu

Bima ya afya ya wafanyakazi wa Kaunti ya Nairobi ya kima cha shilingi bilioni 1.7 iliyopewa kampuni ya AAR imeangaziwa kwa mara nyingine katika ripoti ya Mhasibu Mkuu wa Serikali.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, serikali ya Kaunti ya Nairobi ililipa shilingi milioni 652 zaidi kwa kampuni hiyo.

Hapo jana, wanahabari walizuiliwa kuhudhuria vikao vya Kamati ya Uhasibu wa Umma vya Kaunti hiii chini ya uwenyekiti wa Wilfred Odalo ambapo aliyekuwa Katibu wa serikali ya Kaunti ya Nairobi Leboo ole Morintat ambaye aliidhinisha malipo hayo alikuwa akihojiwa.

Ikumbukwe kuwa hii ni mara ya poli kwa Leboo kuhojiwa na kamati hiyo faraghani.