array(0) { } Radio Maisha | Ajuza mwenye umri wa miaka sitini ni mmoja wa shilingi milioni 72

Ajuza mwenye umri wa miaka sitini ni mmoja wa shilingi milioni 72

Ajuza mwenye umri wa miaka sitini ni mmoja wa shilingi milioni 72

Ajuza mwenye umri wa miaka sitini ni mmoja wa washukiwa wawili waliokamatwa kwa kuhusishwa na wizi wa shilingi milioni 72 za benki ya Standard Chartered tawi la Nairobi West.

Kwa mujibu wa Idara ya Upelelezi, DCU, wawili hao walikamatwa na maafisa wa Kitengo Maalum cha Kukabili Uhalifu na kima cha shilingi milioni mbili, laki tatu na elfu thelathini na tisa kupatikana kutika kwao wakati wa msako nyumbani kwao kwenye eneo la Kalumoni, Kaunti ya Machakos.

Kupitia mtandao wa Twitter, DCI imesema mmoja wa washukiwa hao, John kamau Mulei, ni ndugu ya Bernard Mwendwa ambaye ni afisa wa G4S ambaye alikamatwa baada ya uhalifu huo wiki mbili zilizopita.