array(0) { } Radio Maisha | Mariga kuwania kiti cha ubunge Kibra

Mariga kuwania kiti cha ubunge Kibra

Mariga kuwania kiti cha ubunge Kibra

Sasa ni rasmi kwamba McDonald Mariga atakuwa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mdogo wa Eneo Bunge la Kibra tarehe 7 mwezi Novemba mwaka huu.

Mariga amepata afueni baada ya Jopo la Kusuluhisha Mizozo LA Tume ya Uchaguzi, IEBC chini ya uwenyekiti wa Wafula Chebukati kupuuza suala kwamba angenyimwa fursa hiyo baada ya kusajiliwa siku chache baada ya kiti hicho kutangazwa kuwa wazi.

Aidha, Chebukati anesisitiza kwamba ni jukumu la IEBC kuendelea kuwasajili wananchi kuwa wapigakura muda wowote ule na kwamba licha ya Mariga kusajiliwa katika Eneo Bunge la Starehe, ana uhuru wa kuwania wadhifa wa ubunge eneo la Kibra.

Wakati wa uamuzi huo wa leo, Mariga alikuwa ameandamana na babaye, viongozi kadhaa wa Chama cha Jubilee akiwamo Kiongozi wa Wengi, Aden Duale na mwenzake wa Bunge la Seneti Kipchumba Murkomen.

Mariga aliwasilisha malalamishi Jumatano wiki jana baada ya IEBC kumnyima cheti cha kuwania kiti hicho baada ya jina lake kukosekana katika sajili ya wapiga-kura. Hata hivyo, makamishna wa IEBC wa Starehe alikojisajili Mariga walithibitisha kwamba alijisajiliwa kuwa mpiga-kura tarehe 26 mwezi Agosti hivyo anapaswa kukabidhiwa cheti.