array(0) { } Radio Maisha | washukiwa watatu wa wizi wa magari wanawazuiliwa na Maafisa wa polisi

washukiwa watatu wa wizi wa magari wanawazuiliwa na Maafisa wa polisi

washukiwa watatu wa wizi wa magari wanawazuiliwa na Maafisa wa polisi

Maafisa wa polisi mjini Nakuru wanawazuilia washukiwa watatu wa wizi wa magari. Inaarifiwa washukiwa hao aidha walipatikana na gari linaloaminika kuibwa kutoka kwenye kaunti ya Nyeri.

Naibu Kamanda wa Polisi wa Nakuru Mashariki Ellena Wairimu amesema walipata taarifa kuhusu kuibwa kwa gari hilo na ndipo wakaanzisha uchunguzi .

Washukiwa hao  Stephen Maina, Joseph Kamau na Peter Mwangi watafikishwa mahakamani uchunguzi utakapokamilika.