array(0) { } Radio Maisha | Ndindi Nyoro aomba msamaha kufuatia mvutano na Kamanda

Ndindi Nyoro aomba msamaha kufuatia mvutano na Kamanda

Ndindi Nyoro aomba msamaha kufuatia mvutano na Kamanda

Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro ameomba msamaha kufuatia mvutano kati yake na Mbunge  Maalum Maina Kamanda uliotokea katika kanisa Kikatoliki la Gitui Jumapili iliyopita.

Nyoro amesema amekuwa akikosa amani tangu kushuhudiwa kwa mvutano huo uliotokea wakati wa hafla ya kuchanga pesa, hafla ambayo ilihudhuriwa na viongozi wa kundi la Kieleweka, akisema ilikosesha maana shughuli yenyewe.

Kwa mujibu wa Nyoro hatua yake ya kuomba msamaha imetokana na kwamba hangependa waumini wa kanisa hilo kuanza kudhania ni nani hasa wa kulaumiwa kufuatia sarakasi hiyo, akisema anaomba msamaha kwa niaba ya viongozi wote waliokuwa katika hafla hiyo.

Amesema imefika wakati sasa wa viongozi kuacha kuzungumzia masuala ya siasa makanisani na kwamba wanafaa kuzungumzia mijadala ya kisiasa baada ya ibada, akiahidi kuongoza kwa mfano.