array(0) { } Radio Maisha | Catherine Waruguru awaongoza wakazi kuzua vurugu nje ya kanisa

Catherine Waruguru awaongoza wakazi kuzua vurugu nje ya kanisa

Catherine Waruguru awaongoza wakazi kuzua vurugu nje ya kanisa

Mwakilishi wa Kike wa Laikipia, Catherine Waruguru amewaongoza wakazi wa kaunti hiyo kuzua vurugu nje ya kanisa moja wakati Mbunge Maalumu, Maina Kamanda alikuwa amehudhuria ibada pamoja na viongozi wa Kundi la Kieleweke.

Akiwahutubia wakazi hao, Waruguru aidha amemsuta Kamanda kufuatia mzozo baina yake na Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro.

Amesema Kamanda hana heshima kwani amekuwa akibishana na wabunge ambao si wa umri yake huku akiwashinikiza kuunga mkono kundi lake.

Wakati uo huo, Waruguru amemtaka Kamanda kukoma kuwatusi viongozi wanaomuunga mkono Naibu wa Rais William Ruto.

Amesema ataendelea kumpigia debe Naibu wa Rais katika azma yake ya kuwania urais mwaka wa 2022.