array(0) { } Radio Maisha | Geofrey Kamworor avunja rekodi ya dunia katika mbio za masafa marefu

Geofrey Kamworor avunja rekodi ya dunia katika mbio za masafa marefu

Geofrey Kamworor avunja rekodi ya dunia katika mbio za masafa marefu

Mwanariadha Geofrey Kamworor amevunja rekodi ya dunia katika mbio za masafa marefu ya kilomita ishirini na moja ambazo zilifanyika mjini Copenhagen kwa kuandikisha muda wa dakika hamsini na saba na sekunde hamsini na tisa na kuivunja rekodi ambayo iliandikishwa na mwanariadha Abraham Kiptum ya dakika hamsini na nane na sekunde kumi na nane mjini Valencia mwaka 2018.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka ishirini na sita atakuwa mwanadamu wa kwanza kuwahi kukimbia chini ya dakika hamsini na nane.

Kamworor ambaye ni mshindi wa mbio za masafa marefu ya mwaka 2015 na  2017 aliwahi kuandikisha muda wa dakika hamsini na nane na sekunde hamsini na nne mwaka 2013.