array(0) { } Radio Maisha | ODM yavishtumu vyama tanzu vya Muungano wa NASA
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

ODM yavishtumu vyama tanzu vya Muungano wa NASA

ODM yavishtumu vyama tanzu vya Muungano wa NASA

Uongozi wa Chama cha ODM umevishtumu vyama tanzu vya Muungano wa  NASA kwa kuwateua wawaniaji wa kiti cha ubunge katika eneo la Kibra.

Katibu Mkuu wa ODM, Edwin Sifuna amesema hatua ya viongozi wa vyama vya Ford Kenya na ANC kuwateua wagombea ni kinyume na sheria, hali ambayo anasema inatishia kusambaratika kwa Muungano wa NASA hata zaidi.

Sifuna amewataja Musalia Mudavadi wa ANC na Moses Wetangula wa Ford Kenya kuwa wasaliti na wabinafsi wasiotakia mema ODM.

Amesema uchaguzi huo mdogo wa Kibra utakuwa mwanzo wa kusambaratika kwa NASA kabisa huku vyama vyote vikianza kutafuta uungwaji mkono kwingine.

Ikumbukwe ANC ilmteua Eliud Owalo kupeperusha bendera yake huku Ford Kenya ikimteua Khamisi Butichi kumenyana na Imran Okoth wa ODM. Uchaguzi huo mdogo utafanywa Novemba saba mwaka huu.

Haya yanajiri huku Macdonald Mariga wa Chama cha Jubilee akitarajiwa kujua hatma yake kesho wakati Tume ya Uchaguzi, IEBC itakapotoa uamuzi wa iwapo itampa cheti au la.

Mariga aliwasilisha malalamishi katika Jopo la Kuteua Mizozo katika IEBC Jumatano wiki jana baada ya msimamizi wa uchaguzi kukosa kumkabidhi cheti kwa madai kwamba hajajisajili kuwa mpigakura.