array(0) { } Radio Maisha | Rais Kenyatta ahudhuria ibada ya mazishi ya Robert Mugabe

Rais Kenyatta ahudhuria ibada ya mazishi ya Robert Mugabe

Rais Kenyatta ahudhuria ibada ya mazishi ya Robert Mugabe

Rais Uhuru Kenyatta yuko nchini zimbabwe kuhudhuria hafla ya ibada ya Mazishi kwa heshima ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Robert Mugabe.

Hafla hiyo inayofanyika kwenye Uwanja wa Kitaifa wa Michezo wa Harare inahudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwamo marais wa sasa na wa zamani na inaongozwa na rais Emmerson Mnangawa wa Zimbabwe.

Mbali na Rais Kenyatta baadhi ya viongozi ambao tayari wamewasili Zimbabwe ni Rais wa Namibia Hage Gottfried Geingob mwenzake wa Ethiopia Sahle-Work Zewde, Rais wa Equatorial Guinea  Theodore Obiang Nguema, rais wa Angola João Lourenço, Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Peter Mutharika wa Malawi; Marais wa Zamani wakiongozwa na Thabo Mbeki na Jacob Zuma wa Afrika Kusini, aliyekuwa Rais wa Nigeria Olusegun Obasanjo miongoni mwa wengine.

Hafla hii inajiri baada ya familia ya Mugabe kukubaliana na serikali kuhusu eneo mwili wake utakakozikwa. Mwili wa Mugabe utazikwa kwenye eneo la National Heroes Acre monument jijini Harare. Msemaji wa familia ya Mugabe, Leo Mugabe hata hivyo alisema hawajaafikiana kuhusu siku hasa mazishi yatafanyika baada ya kufutilia mbali mipango ya awali ya kumzika kesho..

Ikumbukwe familia hiyo imekuwa ikivutana na Rais wa sasa Emmerson Munangawa  kuhusu eneo ambapo mwili huo utazikwa baada ya mwili wake kurejeshwa nyumbani Jumatano wiki hii kutoka nchini Singapore alikofariki dunia akitibiwa.

Mugabe alifariki dunia Ijumaa iliyopita baada ya kuugua kwa muda mrefu akitibiwa nchini Singapore. Alikuwa na umri wa miaka tisini na mitano.