array(0) { } Radio Maisha | Seneta Gideon Moi awashauri wakenya kuunga mkono BBI

Seneta Gideon Moi awashauri wakenya kuunga mkono BBI

Seneta Gideon Moi awashauri wakenya kuunga mkono BBI

Huku mjadala kuhusu suala la katiba kufanyiwa marekebisho ukiendelea, Seneta wa Baringo, Gideon Moi kwa mara nyingine amewashauri Wakenya kuunga mkono mapendekezo ya Jopo la Upatanishi, BBI.

Moi ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha KANU amesema BBI ndio pekee ambayo imejukumiwa kutatua mzozo wa uongozi unaoshuhudiwa nchini kila baada ya uchaguzi mkuu.

Akizungumza katika hafla ya mazishi katika eneo la Tongaren kwenye Kaunti ya Bungoma Seneta Moi amewashauri viongozi  kusitisha siasa za mwaka 2022 na badala yake kuwahudumia wakenya ambao waliwachagua.

 

Kwa upande wake Gavana wa Bungoma, Wycliffe Wangamati amesema licha ya kwamba mapendekezo ya Mswada wa Punguza Mizigo yanaonekana kumpendelea Mkenya mlipa-kodi, ni sharti masuala ya Wakenya yaangaziwe kikamilifu.

 

Wakati uo huo,  Mbunge wa Kimilili, Didmus Barasa amesema kwamba licha ya serikali kuweka mikakati ya kuwakabili wafanyabiashara haramu nchini, kuna baadhi ya watu ambao wanawalaghai Wakenya kwa kuwauzia bidhaa ghushi.

Amesema wafanyabiashara hao wamefanya uchumi hasa ya eneo la Magharibi kudorora hivyo wanapaswa kukabiliwa kwa mujibu wa sheria.