array(0) { } Radio Maisha | Mnangawa ayataka mataifa kushinikiza vikwazo dhidi ya Zimbabwe kuondolewa

Mnangawa ayataka mataifa kushinikiza vikwazo dhidi ya Zimbabwe kuondolewa

Mnangawa ayataka mataifa kushinikiza vikwazo dhidi ya Zimbabwe kuondolewa

Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangawa ametoa wito kwa mataifa yaliyoliwekea taifa lake vikwazo kuviondoa kwa heshima ya aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Marehemu Robert Mugabe.

Akihutubu wakati wa hafla ya ibada ya mazishi kwa heshima ya Mugabe Mnangawa amesema vikwanzo hivyo vimeliathiri taifa na kuwaumiza wananchi. Amemtetea Mugabe dhidi ya madai ya uongozi mbaya akisema mataifa yaliyokuwa na chuki na uongozi wake kutoka na misimamo dhidi ya ukoloni ndiyo yaliyochangia taifa hilo kuzorota hasa kiuchumi.

Amesema yu tayari kuendeleza uhusiano mwema na mataifa mengine.

Mnangawa amesifia hatua alizochukuaMgabe kuhakikisha kwmaba ardhi za raia wa Zimbabwe zilizokuwa zimenyakuliwa na wakoloni zimerejeshwa akisema mageuzi katika umiliki wa ardhi aliyoanzisha Mgabe yatalindwa.

Amewashukuru marais wa Afrika waliojitokeza kuhudhuria hafla hiyo akisema Mugabe alilipenda bara hili huku akiwaomba kushirikiana na kuhakikisha umoja miongoni mwao.

Miongoni mwa marais waliohudhuria hafla hiyo ni Rais Uhuru Kenyatta Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na Peter Mutarika wa Malawi miongoni mwa wengine.