array(0) { } Radio Maisha | Ibada ya mzishi ya Mugabe imefanyika, Zibamwe

Ibada ya mzishi ya Mugabe imefanyika, Zibamwe

Ibada ya mzishi ya Mugabe imefanyika, Zibamwe

Hafla ya ibada ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Marehemu Robert Gabriel Mugabe imefanyika Jumamosi. Marais wa sasa na wa zamani wamehudhuria hafla hiyo ya kitaifa ambayo imefanyika katika Uwanja wa Kitaifa wa Michezo wa Harare. Aliyekuwa mwandani wa Kkaribu wa Mugabe na Rais wa kwanza wa Ghana Keneth Kaunda amewaongoza viongozi hao kummiminia sifa kedekede na wamemtaja Mugabe kuwa Baba wa Afrika wakisema aliyajali mataifa ya bara hili na kuyapigania kwa udi na uvumba. Aidha huenda ikachukua muda zaidi kwa mwili wa Mugabe kuzikwa kwani tarehe rasmi ya mazishi hayaafikiwa.

Mmoja baada ya mwingine, Marais wa sasa na wa zamani wa baadhi ya mataifa ya Afrika vilevile viongozi mbalimbali waliwasili katika Uwanja wa Kitaifa wa Harare nchini Zimbabwe kwa ibada ya wafu kwa heshimu ya Rais wa Kwanza wa taifa hilo Marehemu Robert Mugabe.

Wakiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta viongozi hao wamesema alipokuwa uongozini Mugabe alipigania uhuru wa mataifa ya Afrika na kuhakikisha kuwa ukoloni mambo leo unatokomezwa.

Rais Kenyatta amesema Marehemu Mugabe hakuogopa kuwakabili wapinzani waliolenga  kuiangamiza Afrika na aliamini ilikuwa na raslimali zinazoweza kuyaendeleza bila kuyategemea mataifa mengine.

Wakati uo huo, Rais Uhuru Kenyatta amewapa changamoto viongozi wa Afrika kuweka maslahi ya wananchi wao mbele alivyofanya Marehemu Mugabe.

Rais wa sasa wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa kwa upande wake ametoa wito kwa mataifa yaliyoliwekea taifa lake vikwazo kuviondoa kwa heshima ya Mugabe.

Amemtetea Mugabe dhidi ya madai ya uongozi mbaya akisema mataifa yaliyokuwa na chuki na uongozi wake kutokana na misimamo dhidi ya ukoloni ndiyo yaliyochangia taifa hilo kuzorota hasa kiuchumi.

Amesema yu tayari kuendeleza uhusiano mwema na mataifa mengine.

Mnangagwa amesifia hatua alizochukua Mugabe kuhakikisha kwamba ardhi za raia wa Zimbabwe zilizokuwa zimenyakuliwa na wakoloni zimerejeshwa akisema mageuzi katika umiliki wa ardhi aliyoanzisha rais huyo wa kwanza yatalindwa.

Aliyekuwa Rais wa Ghana Jerry John Rawlings amesema vikwazo dhidi ya Zimbabwe havikufaa na kuyashtumu vikali mataifa yaliyofanya kila kuhudu kulirejesha nyuma taifa hilo.

Kinyume na ilivyotarajiwa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa hakualikwa kuhutubu. Aidha tofauti za muda mrefu ambazo zimekuwapo baina ya Zimbabwe na Uingereza na hata Marekani zilithihirika wazi ,kwani hakuna viongozi wa juu walioalikwa kuhutubu.

Hata hivyo wawakilishi wa Urusi na Uchina walihutubu.

Viongozi wengine ambao wamehudhuria hafla hiyo ni Rais wa Malawi Peter Mutarika na Theodoro Obiang wa Equitorial Gunea. Marais wa zamani waliokuwapo kwenye hafla hiyo ni Jacob Zuma na Thabo Mbeki wa Afrika Kusini. Mwingine ni aliyekuwa Rais wa Nigeria Olusegun Obasanjo.

Hata hivyo,  haijaafikiwa kuhusu siku rasmi ambapo mwili wa marehemu Mugabe utazikwa huku Rais Mnangawa akisema wataheshimu uamuzi wa familia.

Hapo jana serikali na familia ya Mugabe waliafikiana kwamba mwili huo utazikwa katika eneo la National Heros Monument jijini Harare.

Mugabe aliyeliongoza taifa hilo kwa miaka thelathini na saba alifariki dunia Ijumaa iliyopita akitibwa nchini Singapore baada ya kuugua kwa muda mrefu. Alikuwa na umri wa miaka tisini na mitano.