array(0) { } Radio Maisha | Mwili wa raia wa Uholanzi Tobs Cohen wapatikana

Mwili wa raia wa Uholanzi Tobs Cohen wapatikana

Mwili wa raia wa Uholanzi Tobs Cohen wapatikana

Na Caren Papai

NAIROBI, KENYA, Mwili wa raia wa Uholanzi, Tobs Cohen aliyeripotiwa kutoweka katika hali ya kutatanisha umepatikana ndani ya tangi la maji mtaa wa Lower Kabete, kaunti ya Kiambu.

Tayari polisi wamekita kambi katika eneo la Farasi Lene lililoko boma lake ili kufanikisha uchunguzi wa kufuatia kisa hicho.

Tobs aliripotiwa kutoweka katika boma lake kati ya 19 na 20 mwezi Julai mwaka huu akiwa na mkoba wake japo haikufahamika alikokuwa akienda.

Akihojiwa na wanahabari baada ya mwendazake kutoweka siku ya tarahe 9 mwezi uliopita, mkewe marehemu Sarah Wairimu Kamotho alisema kwamba mumewe alikuwa amelalamikia kuwapo kwa mawakili waliokuwa wakitaka fedha kutoka kwake.

Ikumbukwe mkewe, amekuwa akichunguzwa kufuatia kutoweka kwa Cohen.