array(0) { } Radio Maisha | Rastafari ni dhehebu sawa na mengine, Mahakama Kuu yaamuru

Rastafari ni dhehebu sawa na mengine, Mahakama Kuu yaamuru

Rastafari ni dhehebu sawa na mengine, Mahakama Kuu yaamuru

Na Mate Tongola

NAIROBI, KENYA, Mahakama Kuu imeamuru kuwa Rastafari ni dhehebu sawa na mengine.

Katika uamuzi wake Jaji Chacha Mwita amesema watu wa dhehebu hilo hawafai kubaguliwa kutokana na imani zao. Uamuzi huo unafuatia kesi iliyowasilishwa na mwanafunzo mmoja wa Shuel ya Upili ya Olympic aliyefurushwa shuleni na kuagizwa kuzikata nywele zake. Jaji Mwita agizo hilo ni kinyume cah sheria na linakiuka haki za mwanafunzi huyo..

Mwanafunzi huyo aliwasilisha kesi mahakamani kupitia babake aliyesema kuwa hatua ya shule hiyo ni ubaguzi kwa mwanawe.

Ikumbukwe kulingana na kipengele cha thelathini sehemu ya kwanza ya katiba ni kwamba kila mtu ana huru wa kuabudu.