array(0) { } Radio Maisha | KUPPET yapinga takwa la Shahada ya Uzamili kwa Walimu Wakuu

KUPPET yapinga takwa la Shahada ya Uzamili kwa Walimu Wakuu

KUPPET yapinga takwa la Shahada ya Uzamili kwa Walimu Wakuu

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Chama cha Walimu wa Shule za Upili na Vyuo vya Kadri, KUPPET kimepinga takwa la Tume ya Huduma za Walimu TSC, kwamba watakaotuma maombi ya kutaka kuwa walimu wakuu au manaibu walimu wakuu sharti wawe na Shahada ya Uzamili (Masters Degree).

Katibu Mkuu wa KUPET Akello misori ameiokosoa TSC akisema kwmaba si walimu wote walio na shahada hiyo ya uzamili na ambao wana uwezo wa kushikilia nyadhfa hizo. Misori aidha amesema kwamba takwa hilo litawafungia nje walimu wengi walio natajriba ya hali ya juu katika kazi .

Japo chsma hicho kimesema hakipingi kuajiriwa kwa walimu kwa kuangazia hali yao ya somo, wameitaka TSC kuzingatia masuala mengine muhimu miongoni mwa walimu.

Chama hicho sasa kimeiandikia tume hiyo kikiitaka uiondoe takwa hilo, huku kikitarajiwa kufanya mkutano wiki ijayo kuhusu suala hilo.