array(0) { } Radio Maisha | Mariga kubaini hatma yake Jumatatu

Mariga kubaini hatma yake Jumatatu

Mariga kubaini hatma yake Jumatatu

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA,

Tume ya Uchaguzi, IEBC Jumatatu ijayo uamuzi wa iwapo Macdonald Mariga, mgombea wa Jubilee wa uchaguzi mdogo wa Kibra ataidhinishwa kuwania kiti hicho au la.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati, uamuzi huo utatolewa mwendo wa saa nne asubuhi.

Jopo hilo linaongozwa na Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati na Makamishana Abdi Guliye na Boya Mulu vile vile Katibu amabye atakuwa mwanasheria. Baada ya kusikiliza malalamiko ya Mariga jopo hilo linatarajiwa kutoa mwelekeo wa iwapo Mariga anastahili kuwania wadhfa huo au la.

Mariga aliwasilisha malalamiko yake siku ya Jumatano baada ya IEBC kumnyima idhini ya kuwania wadhfa huo kwa madai kuwa jina lake halikuwapo katika sajili ya wapigakura. Hata hivyo, Mariga kupitia mawakili wake amepinga madai hayo akisema kwamba alikuwa amejisajili kuwa mpigakura katika kituo cha Starehe na kwamba kuzuiwa kwake kunachochewa na washindani wake wa kisiasa.

Hayo yanajiri huku baadhi ya waliowasiliha maombi wakitaka kuipeperusha bendera ya Jubilee wakiapa kupinga uteuzi wa Mariga, huku wakisema ulitekelezwa pasi na kufuata sheria.

Wakiongozwa na Rajab Elli Omondi sasa wanaitaka Bodi ya Uchaguzi ya Jubilee kuvunjwa kwa kukiuka sheria za chama. Wawili hao tayari wamewasilisha malalamishi yao kwa kamati maalum ya kutatua mizozo ya chama cha Jubilee.

Ikumbukwe IEBC ina siku saba za kumuidhinisha au kutomuidhinisha Mariga kuwania wadhfa huo katika uchaguzi mdogo utakaofanyika tarehe 7, mwezi Novemba.