array(0) { } Radio Maisha | Serikali imepiga marufuku raia wa kigni kuasili ''adopt'' watoto humu nchini

Serikali imepiga marufuku raia wa kigni kuasili ''adopt'' watoto humu nchini

Serikali imepiga marufuku raia wa kigni kuasili ''adopt'' watoto humu nchini

Raia wa kigeni hawataruhusiwa kuwaasili (adopt) watoto huku nchini. Serikali imetangaza kupiga marufuku uasili wa watoto ambao ni raia wa Kenya na raia wa kigeni. Wakati wa kikao cha Baraza la Mawaziri Wizara ya Leba imeagizwa kubuni sera mpya zitakazoongoza mchakato huo.

Mbali na kubuni mikakati itakayoongoza taasisi muhimu zinazowalinda watoto humu nchini.

Agizo hili limetolewa siku moja tu baada ya taasisi inayoshughulikia maslahi ya watoto nchini Child Wellfare Society of Kenya kuwaruhusu raia wa Marekani kumchukua mwanao waliyemwasili ambaye ni raia wa Kenya.

Kisa hiki kimeibua mvutano hasa baada ya kuipotiwa kwamba wawili hao walikuwa anajihusisha katika ulanguzi wa watoto madai waliyoyakana vikali na hata kuwasilisha kesi mahakamani wakitaka kurejeshewa mwanao, anayejulikana kwa jina Baby Kiano.

Kwa sasa mtu yeyote aliye kati ya umri wa miaka ishirini na mitano hadi sitini na mitano anaruhusiwa kuasili mtoto humu nchini mradi awe ametimiza masharti yanayohitajika kisheria. Kwa mfano; sharti awe na miaka ishirini na mmoja zaidi ya anayetaka kumuasili.

Kulingana na kipengele cha  mia moja hamsini na nane sehemu ya tatu kwa sasa mtu anaweza kunyiwa kuasii mtoto iwapo tu ; hana akili timamu, amewahi kuhukumiwa kutokana na makosa yoyote, iwapo anajihusisha katika uhusiano wa jinsia moja, na iwapo ni mwanaume pekee.