array(0) { } Radio Maisha | Serikali imepiga marufuku raia wa kigeni kuwaasili (adopt) watoto nchini

Serikali imepiga marufuku raia wa kigeni kuwaasili (adopt) watoto nchini

Serikali imepiga marufuku raia wa kigeni kuwaasili (adopt) watoto nchini

Serikali imepiga marufuku raia wa kigeni kuwaasili, adopt watoto nchini. Uamuzi huo umeafikiwa wakati wa Baraza la Mawaziri lililoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta. Wakati uo uo, Wizara ya Leba imeagizwa kubuni sera mpya zitakazoongoza mchakato huo.

Mbali na kubuni mikakati itakayoongoza taasisi muhimu zinazowalinda watoto humu nchini.

Agizo hili limetolewa siku moja tu baada ya taasisi inayoshughulikia maslahi ya watoto nchini Child Wellfare Society of Kenya kuwaruhusu raia wa Marekani kumchukua mwanao waliyemwasili ambaye ni raia wa Kenya.

Kisa hiki kimeibua mvutano hasa baada ya kuipotiwa kwamba wawili hao walikuwa anajihusisha katika ulanguzi wa watoto madai waliyoyakana vikali na hata kuwasilisha kesi mahakamani wakitaka kurejeshewa mwanao, anayejulikana kwa jina Baby Kiano.