array(0) { } Radio Maisha | Wakenya ni miongoni mwa watu 300 ambao wamekamatwa kufuatia ulaghai wa mitandaoni

Wakenya ni miongoni mwa watu 300 ambao wamekamatwa kufuatia ulaghai wa mitandaoni

Wakenya ni miongoni mwa watu 300 ambao wamekamatwa kufuatia ulaghai wa mitandaoni

Watu mia tatu wakiwamo Wakenya wamekamatwa kufuatia oparesheni ya kimataifa inayowalenga walaghai wa mitandaoni.

Inaarifiwa miongoni mwa waliokamatwa ni raia mia moja sitini na saba wa Nigeria, sabini na wanne wakikamatwa nchini Marekani, kumi na wanane nchini Uturuki na kumi na watano nchini Ghana. wengie wamekamatwa katika mataifa ya Italia, Japan, Malesyia na Uigereza.

Taarifa ya kitengo cha Haki nchini Marekani imedokeza kwamba washukiwa hao ni wanachama wa mtandao wa ulahai ulioanzishwa nchini Nigeria na sasa umesambaa hadi katika amtaifa mengine.

Oparesheni hiyo imechukua kipindi cha miezi minne. Aidha, wakati wa oparesheni hiyo maafisa walioiongoza walifanikiwa kupata dola milioni 3.7 ambazo ni sawa na shilingi milioni mia tatu themanini na nne za Kenya.