array(0) { } Radio Maisha | Wafanyakazi wa Idara ya Mahakama walioshtakiwa kwa kuiba heroine waaachiliwa huru

Wafanyakazi wa Idara ya Mahakama walioshtakiwa kwa kuiba heroine waaachiliwa huru

Wafanyakazi wa Idara ya Mahakama walioshtakiwa kwa kuiba heroine waaachiliwa huru

Maafisa watatu wa Idara ya Mahakama waliofunguliwa mashtaka ya kuhusika na wizi wa dawa za kulevya aina ya heroine yenye thamani ya shilingi milioni 30, wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki saba kila mmoja wao au mdhamini wa kiwango sawa na hicho.

Kuachiliwa kwao kunajiri siku mbili tu baada ya Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Mombasa, Edgar Kagoni kuwaachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja baada ya kuwasilishwa mbele ya Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Nairobi, Lucas Onyina.

Kagoni aliaachiliwa baada ya Mahakama Kuu ya Mombasa kuagiza kuachiliwa kwake kwa bondi ya shilingi laki moja au pesa taslimu shilingi elfu 20 kadhalika kuagiza kutoshtakiwa kwake kwa kuhusishwa na heroin.

Kwa mujibu Hakimu Lucas Onyina, kesi dhidi ya Kagoni itaendelea hadi wakati ambapo stakabadhi halisi zitakapowasilishwa mbele yake.