array(0) { } Radio Maisha | Polisi wanachunguza wizi wa pesa, Moyale
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Polisi wanachunguza wizi wa pesa, Moyale

Polisi wanachunguza wizi wa pesa, Moyale

Kufikia sasa idara ya polisi haijaweka wazi kiwango cha fedha za benki ya Equity ambazo ziliibiwa na wezi mjini Moyale jana alasiri.
Inaarifiwa kwamba wezi hao waliojihami walivamia Uwanja Mdogo wa Ndege wa Moyale na kuwapora maafisa wa polisi waliokuwa wakisafirisha fedha hizo kutoka Nairobi kuelekea Moyale.

Kesi hiyo iliripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Moyale mwendo wa saa saba unusu.

Tukio hilo liliripotiwa na Sejenti Mkuu Galvacioh Marigu ambaye alikuwa amewasindikisha maafisa wa Benki hiyo kuelekea katika Uwanja Mdogo wa Ndege wa Odda takriban kilomita kumi kutika kituo hicho cha polisi ili kuwapa ulinzi baada ya fedha hizo kuwasili kwa ndege.

Aidha, imeripotiwa kwamba Rubani wa Ndege hiyo Alex Kirate, msaidizi wake Johne Michael Onunga na afisa wa fedha katika Kampuni ya Wells Farhi Nelson Langat Kipngetich walishambuliwa na washukiwa hao wa wezi ambao walikuwa wamejihami kwa bastola na ambao waliwashurutisha kulala chini kabla ya kupokonywa sanduku iliyokuwa imebebea fedha hizo.

Kisa hiki kinajiri wiki moja tu baada ya wahalifu kuvamia benki ya Standard Chartered tawi la Nairobi West ambako walitoweka na shilingi milioni 72.

Hata hivyo, washukiwa hao; Chris Machogu,  Duncan Kaveshi Luvuga, Boniface Mutua, Vincent Owuor, Alex Mutuku na Francis Muriuki, walikana mashtaka dhidi yao walipofikishwa mahakamani mapema jana. 

Hakimu wa Mahakama ya Milimani - Francis Andayi,  aliwaachili washukiwa hao wakiwamo maafisa watatu wa polisi kwa bondi ya shilingi milioni moja huku akiwataka kuripoti kila siku kwa siku saba katika makao makuu ya Idara ya Upelelezi, DCI. 

Kesi hiyo itatajwa tena Septemba 23 .