array(0) { } Radio Maisha | Polisi wanachunguza kuuliwa kwa wanaume 2 imepatikana Kibirichi, Nyamira

Polisi wanachunguza kuuliwa kwa wanaume 2 imepatikana Kibirichi, Nyamira

Polisi wanachunguza kuuliwa kwa wanaume 2 imepatikana Kibirichi, Nyamira

Polisi wanatarajiwa kuanzisha uchunguzi kufuatia kupatikana kwa mili ya wanaume wawili ambayo imepatikana kwenye eneo la Kibirichi mpakani pa Kaunti za Nyamira na Kisii.

Mili hiyo imepatikana ikiwa na majeraha huku chifu wa eneo hilo, Moses Ochanga akisema huenda waliuliwa kwingine kabla ya kutupwa eneo hilo.

Katika kisa tofauti, mwili uliokuwa na majeraha kwenye kichwa umeptikana kwenye Kijiji cha Gesara Kitutu Chache Kaunti ya Kisii.

Kwingineko, mwili wa mwanamume wa umri wa miaka 28 umepatikana katika shamba la mahindi kwenye eneo la Kipyeto, Eneo Bunge la Mlima Elgon. Inasemakana kwamba jamaa huyo aliuliwa na watu wasiojulikana. Alionekana mara ya mwisho tarehe 25 mwezi uliopita huku uchunguzi ukiendelea kufuatia kisa hicho.