array(0) { } Radio Maisha | Sossion amepigwa marufuku kuingia katika ofisi za KNUT
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Sossion amepigwa marufuku kuingia katika ofisi za KNUT

Sossion amepigwa marufuku kuingia katika ofisi za KNUT

Licha ya Katibu Mkuu wa Chama cha Kitaifa cha Walimu KNUT, Wilson Sossion kupata agizo la mahakama kuzuia kufurushwa kwake kutoka chama hicho, masaibu dhidi yake yanaendelea kuongezeka baada ya kamati kuu ya usimamizi KNUT kumpiga marufuku katika makao makuu yake.

Mwenyekiti wa KNUT, Wilson Omucheyi amesisitiza kuwa Sossion alisita kuwa msemaji wa KNUT pindi alipondolewa katika sajili yao. Omucheyi amesisitiza uamuzi wao wa Agosti 29 kumteua Hesbon Otieno kuwa Kaimu Katibu Mkuu akisema jina la Otieno lingaliwa limesajiliwa na msajili wa vyama kuwa katika wadhifa huo.

Kauli hii imetiliwa mkazo na Mweka Hazina wa Kitaifa John Matiang'i ambaye amemtaka Sossion kuheshimu maamuzi ya chama hicho.

Viongozi hao vilevile wamedokeza kuwa watashiriki mkutano na Tume ya Huduma za Walimu TSC leo kujadili masuala tata yakiwamo kuwarejesha walimu waliaochishwa kazi, kulainisha ulipaji mshahara baada ya TSC kuanza kuwalipa baadhi ya walimu pasi na nyongeza wala marupurupu waliyoafikiana na kadhalika.

Ikumbukwe ni juzi tu Sossion alipohutubia kikao cha wanahabari akiwa na baadhi ya maafisa wa KNUT mashinani walioapa kusimama naye.