array(0) { } Radio Maisha | Jubilee kufanya mkutano wa dharura kufuatia kuondolewa kwa Maiga kinyang'anyironi
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Jubilee kufanya mkutano wa dharura kufuatia kuondolewa kwa Maiga kinyang'anyironi

Jubilee kufanya mkutano wa dharura kufuatia kuondolewa kwa Maiga kinyang'anyironi

Chama cha Jubilee kimeitisha mkutano wa dharura wa  wanachama wa bodi ya uchaguzi na maafisa wengine wanaoshirikiana nao chamani ili kuamua hatma ya mgombeaji wao katika uchauzi mdogo wa Kibra, Macdonald Mariga.

Katibu Mkuu wa Jubilee Raphael Tuju amesema wakati wa mkutano huo uwatatathmini utata ulioibuka kufuatia hatua ya Tume ya Uchaguzi Nchini IEBC kumyima idhini ya kuwania kwa kukosekana katika sajili ya wapiga kura itakayotumika wakati wa uchaguzi huo mdogo. Tuju amezungumza muda mchache baada ya Mariga kuwasilisha malalamishi mbele ya jopo la kutatua mizozo la IEBC.

Katika malalamiko hayo, Mariga amesema alisajiliwa kuwa mpigakura katika kituo cha Karikor eneo bunge la Starehe tarehe 26 Agosti takriban wiki mbili baada ya kiti cha ubunge kutangazwa kuwa wazi na hivyo usajili wa wapigakura kusimamishwa. Kapitia Kampuni ya Uwakili ya Majimbo and Co, Mariga amesema hatua ya kunyimwa idhini ya kuwania ni kumnyima haki yake. Oliver Kipchumba ni wakili.

Jopo hilo linatarajiwa kumwita Mariga kufikia kesho ili kumsikiliza kabla ya kutoa uamuzi chini ya kipindi cha siku saba kuanzia aliponyimwa idhini juzi. Hayo yanajiri huku sasa ikibainika kwamba  hakuna Mkenya aliyesajiliw abaada ya uchaguzi wa mwaka 2017 ameruhusiwa kushiriki chaguzi ndogo mbazo zimefanyika zikiwamo za Embakasi Mashariki na Ugenya.

Hatua hii ni kutokana na utaratibu unaostahili kufuatwa wa sajili kuidhinishwa upya na kuchapishwa katika gazeti rasmi la serikali jambo ambalo halijafanyika.

Hata hivyo baadhi ya maafisa chamani Jubilee wanateta kwamba utaratibu wa serikali haufai kumtatiza mpigakura kwa mujibu wa katiba.