array(0) { } Radio Maisha | Bangi yenye thamani ya shilingi 860,000 yanaswa Kitui

Bangi yenye thamani ya shilingi 860,000 yanaswa Kitui

Bangi yenye thamani ya shilingi 860,000 yanaswa Kitui

Maafisa wa polisi mjini Kitui wamewanasa washukiwa 4 wa ulanguzi wa dawa za kulevya.

Washukiwa hao wamekamatwa wakiwa na bangi yenye thamani ya shilingi 860,000 katika eneo la Kibwezi

Kamanda wa Makueni Joseph ole Napeiyan amesema bangi hiyo yenye uzani wa kilogramu mia mbili na moja, ilikuwa imeletwa sehemu hiyo na washaukiwa watatu wa kutoka kaunti ya Migori.

Bangi hiyo ilikuwa imefichwa katika nyumba ya mwanamke mmoja ambaye pia amenaswa kufautia tukio hilo.

Gari dogo aina ya Saloon ambalo linadaiwa kutumika katika usafirishaji wa bangi hiyo limezuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kibwezi..